Monday, January 6, 2025

MTAALA MPYA ELIMU MSINGI 2023



 Mtaala na Mihtasari ya Elimu Msingi · Curriculum for Primary Education Standard I - VI · Mtaala wa Elimu ya Msingi Darasa la I - VI

BOFYA HAPA KUPAKUA

BOFYA HAPA KUPAKUA

BOFYA HAPA KUPAKUA

BOFYA HAPA KUPAKUA

BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA NNE (4) 2024

 

 Katibu Mkuu Baraza la Mitihani Tanzania NECTA ametangaza matokeo ya darasa la nne mwaka 2024.

Kuangalia Ingia hapa

MATOKEO LINK 1

MATOKEO LINK 2

Saturday, January 4, 2025

BARAZA LA MITIHANI LATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024

 


Katibu Mkuu Baraza la Mitihani Tanzania NECTA ametangaza matokeo ya kidato cha pili mwaka 2024.

Kuangalia Ingia hapa

MATOKEO LINK 1

MATOKEO LINK 2


Tuesday, December 31, 2024

_MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:_

 _MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:_



_1.Mtihani wa darasa la Saba utafutwa._


 _2.Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize Kidato cha nne._


_3.Kutakuwa Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (STANDARD SIX NATIONAL ASSESSMENT)._


_4.Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza Kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza._


_5.Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa kama somo kwa Shule za Kiswahili Medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa Shule za English Medium._


_6.Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 tofauti na ya sasa miaka 7._


_8.Elimu ya Awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5._ 


_9.Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa ni KKK, Jiografia,kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati,Sayansi, historia ya TANZANIA na Maadili,Dini na kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa._


_10.Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza._


_11.Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa._


_12.Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na Amali (Ufundi)._ _Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo,matakwa na malengo yake ya baadaye._ 


_13.Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:-_

_Kilimo na Ufugaji._

_Umakenika._

_Biashara na Ujasiriamali._

_Sanaa na Ubunifu._

_Elimu ya Michezo._

_Ufugaji wa Nyuki._

_Uchimbaji wa Madini._

_Urembo._


_14.Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua Masomo manne (4) ya jumla na moja la fani._


_15.Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:-_

_Hisabati._

_Elimu ya Biashara._ 

_Kiingereza._

_Historia ya Tanzania na Maadili._


_16.Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili yaani:-_

_Cheti cha ujumla cha Elimu ya Sekondari (NECTA) na Cheti cha Amali ( NACTIVET)._


_17.Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi._


_18.Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi,hii ni kwa ajili ya Ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika._


_19.Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (ACADEMIC COMMUNICATION) katika A-level na Ualimu._ 


_20.CODING itafundishwa Shule za Msingi._


_21.INFORMATION and COMPUTER STUDIES (ICS) itabadilishwa na kuitwa COMPUTER SCIENCE.Somo limesukwa upya._ 


_22.CIVICS itaunganishwa na Historia ya TANZANIA na Maadili kwa O-level._ 


_23.O-level Masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa._ 


_24.Katika O-level Masomo ya Biology na Geography yatakuwa Masomo ya kuchagua pia kwa sababu Maudhui yake yamekuwa kwenye Masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi kwa mfano Afya ya Jamii,Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi nk._


_25.Civics, Maarifa ya Jamii,Uraia na Maadili yamefutwa, Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya TANZANIA na Maadili._


_26.General Studies (GS) katika A-level itafutwa na Maudhui yake yatawekwa katika Somo la Historia ya TANZANIA na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma._


_27.Kufuta baadhi ya Masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudiarudia kwa Maudhui._


_28.Michepuo katika Elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9)._ 


_Michepuo iliyoongezeka ni:-_

_Sanaa._

_Lugha._

_Muziki._

_Michezo._

_Tehama._


_29.Masomo ya O-level yatakuwa:-_

_Biology._

_Physics._

_Chemistry._

_History._

_Geography._

_Historia ya TANZANIA na Maadili._

_Hisabati._

_Kiswahili._

_English._

_Elimu ya Biashara._

_Utunzaji wa _Taarifa za Fedha._

_Computer Science._

_Bible Knowledge._

_Elimu ya Dini ya kiislamu etc._


_30.Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (DIPLOMA) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu._


_Watakaosoma Stashahada watakuwa waliomaliza Kidato cha Sita na itasomwa kwa miaka miwili._ 


_31.Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (DEGREE). kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu._


_32.Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (DIPLOMA) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa continuous Professional Development._

Wednesday, December 25, 2024

Mh Rais Wa Tanzania atema nyongo kuhusu Elimu ya Tanzania

 



Tuesday, December 24, 2024

Merry Christmas

 


It's hopefully  that all students and pupils are together with your parents.

As onliteacher zone we send our gratitude merry Christmas  to all all.

Whilst at this make time relax for brain before getting back for classes resume.

Some of your will be Candidate Class and some of are getting into secondary school which is a step towards learning and getting matured.

MERRY CHRISTMAS 🤶 🎄 ❤️ AND HAPPY NEW YEAR 2025